Katika kusherekea miaka kumi na saba toka kuanzishwa kwa East Africa Radio, mbali na burudani zinazoendelea kufanyika kila mwisho wa wiki katika jiji la Dar es Salaam
sasa East Africa Radio inarudisha fadhila kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari, pikipiki, bajaji kwa kukujazia mafuta kwenye chombo chako cha usafiri.
Kampeni hii inatarajia kuanza rasmi katika jiji la Dar es Salaam leo, ili kuweza kupata bahati ya kujaziwa mafuta kwenye chombo chako cha usafiri ni wewe msikilizaji wa East Africa Radio kuendelea kusikiliza Radio kupitia masafa ya 88.1 FM kwa jiji la Dar es Salaam. Ambapo 'Kachero' atakuwa anatoa maelekezo kupitia Radio kuwa yupo katika kituo gani cha mafuta na ukiweza kufika kituo hicho kwa muda huo atakujaza na wesi kwenye chombo chako.
Msimamizi Mkuu wa vipindi vya East Africa Radio, Nasser Kingu amesema kuwa lengo kubwa la kampeni hii ni kuendelea kuwashukuru na kusherehekea na vijana na wasikilizaji wa East Africa Radio ambao wamekuwa wakiwapa ushirikiano wa kutosha kwa miaka kumi na saba toka kuanzishwa kwa kituo hicho.
"Tunaendelea kusherekea miaka kumi na saba ya East Africa Radio na vijana na wasikilizaji wetu, kama tunavyofahamu Makachero walikuwepo mitaani katika jiji la Dar es Salaam ambapo waliweza kugawa mihela na zawadi mbalimbali kwa watu waliowakuta wakisikiliza East Africa Radio. Kwa sasa tunawajaza wasikilizaji wetu na mafuta katika vyombo vyao vya usafiri, wenye daladala, magari binafsi, bajaji, bodaboda hata malori kwani tunatambua mafuta yatawawezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine hivyo tumeona tusherekee nao kwa kuwajaza wesr" alisema Nasser Kingu
Mbali na hilo Nasser Kingu alisisitiza kuwa kampeni hiyo ya kuwajazia watu mafuta kwenye vyombo vyao vya moto itafanyika kwa jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa itafanyika kila pande za jiji la Dar es Salaam ili kuwafikia watu wote ambao ni wasikilizaji wa East Africa Radio. Msimamizi huyo wa vipindi kutoka East Africa Radio amewataka watu wa Dar es Salaam kuendelea kusikiliza vipindi bora vilivyoandaliwa kwa ufanisi mkubwa kupitia 88.1 FM ili kufahamu namna nzuri itakayo tumika kuwawezesha wasikilizaji kujazwa na mafuta kutoka kwa makachero wa East Africa Radio.