Tanzania yaporomoka viwango Fifa
TANZANIA imeporomoka kwa nafasi tano kwenye viwango vya ubora wa soka duniani kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotolewa jana na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).
Viwango hivyo vinaonyesha kuwa Tanzania sasa iko nafasi ya 130 kutoka 125 iliyokuwa awali wakati viwango vya mwisho vilipotolewa Machi mwaka huu.
Januari mwaka huu, Tanzania ilikuwa nafasi 126, wakati Februari ilipanda kwa nafasi moja hadi 125.
Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, Rwanda na Burundi ndizo pekee zilizopanda viwango.
Rwanda imepanda kwa nafasi moja hadi 87, wakati Burundi imepanda kwa nafasi saba na sasa iko namba 122.
Kenya imeporomoka zaidi kwa nafasi 12 na kushika namba 115, huku Uganda nayo ikishuka chini kwa nafasi tano na kushinda namba 72.
Algeria bado inaongoza kwa upande wa Afrika wakipanda kwa nafasi nne hadi nafasi ya 33.
Kama ilivyotegemewa Argentina kuipiku Ubelgiji kwa viwango vya ubora, ndivyo ilivyotokea safari hii wakipanda kwa nafasi moja Ubelgiji wako nafasi ya pili, wakati England wakiporomoka nafasi moja na kufunga 10- ora.
Chile wako nafasi ya tatu, wakifuatiwa na Colombia, huku Ujerumani wakishika nafasi ya tano.
Hispania wanashika nafasi ya sita, wakifuatiwa na Hispania, huku Brazil wakiporomoka kwa nafasi moja hadi namba saba, Ureno nafasi ya nane na Uruguay nafasi ya tisa.