Kanumba uliondoka na bongo movie yako

Ikiwa leo ametimiza miaka minne toka alipofariki dunia Apr 7, 2012 Msanii wa filamu nchini Steve Kanumba, baadhi ya mashabiki wa filamu na wadau wa mbalimbali wamezidi kuonesha kuwa pengo lililoachwa na Kanumba kwenye tasnia ya filamu nchini linazidi kuongezeka zaidi badala ya kupungua.

Mategemeo ya watu wengi ni kuona kiwanda cha filamu nchini kinakuwa zaidi na kuweza kuwa na mafanikio zaidi, lakini wao wakilinganisha hatua ambayo tayari Kanumba alikuwa amepiga mpaka anafikwa na umauti na hali iliyopo sasa wanaona ni kama wanarudi nyuma badala ya kwenda mbele.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa East Africa Radio ambao wameweka wazi mtazamo wao na maoni yao juu ya tasnia ya movie nchini na kifo cha Kanumba.

"R.I.P. The Great ila huko uliko tambua uliondoka na Bongo movie yako, huku wamebaki makanjanja tu hata yule swahiba wako kumbe si lolote pasipo kampani yako" Martin Nzumbe
"R.I.P Kanumba,lakini huku Bongo movie imekuwa fagilia mafisadi tu, na harufu ya ngono hakuna kingine." Amos Masusu

"Baba yao wa Bongo movie ametutoka sasa wamebaki yatima na wajane wengine wanakazi ya kujichubua R.I.P Kanumba mbele yako nyuma yetu" Beni Magaya
"Kanumba The great Hope movie zako zinaendelea kutisha up to this moment hakuna kama wewe hapa bongo uliondoka na hii tasnia nzima ya Bongo movie zimebaki mbwembwe tu" Amon Shimba

"R.I.P Kanumba muda mwingine nakata tamaa hata kuangalia hizi filamu za sasa maana kichefuchefu ila tumani limebaki kwa JB na Gabo labda. Maana hata hawa waliopewa tuzo awana viwango vyako.
Je nani atakuja kuitikisa filamu kama wewe? hakuna tena labda mwanangu". Robert Steven

About Admin

0 comments:

Post a Comment