wanakomaa kwenye simu na kompyuta kumbuka hata vioo hivyo vina mazara tuu pale unapo
vikaribia.
Simu zetu watoto au wadogo zetu wanaweza wakawa wanazitumia kama vifaa vya kusababisha
furaha yao, wanaweza wakaamua kucheza michezo mbali mbali na mda mwingine wanaweza
wakatumia kama njia ya kusomea. Sasa utawezaje kuwaweka mbali na kioo cha kifaa
wanachotumia
Shukrani kwa Samsung ambao wamekuja na App inayojulikana kama Safety Screen, hii inatumia
teknolojia ya kugundua sura (facial recognition). App hii itagundua kama mtumiaji wa kifaa hicho
yuko karibu na kioo cha kifaa.
Kama mtumiaji akiwa karibu na kioo basi kitatokea kikatuni, ambacho kitamjulisha mtumiaji kwamba
yupo karibu na kioo cha kifaa na hivyo inabidi arudi nyuma. Endapo mtumiaji atakapoungeza
umbali wa kutoka alipo na kifaa hicho basi hicho kikatuni kitaondoka, kumjulisha kwamba
yupo umbali sahihi.
Samsung wametengeza App hii wakiwa na madhumuni mengi. Zuri kati ya madhuni hayo
ni kwamba App hii itamjenga mtoto kujua njia nzuri ya umbali wa kutumia pale
anapotumia vitu vya kielektroniki kama vile Tv.
Kumbuka kama mtu akiwa anatumia muda mwingi sana katika kuangalia kitu katika skrini ana
hati hati ya kuharibu macho yake na hiyo ikiwemo kuharibu uwezo wake wa kuona kabisa.
Cha kufanya ni kupakua App hii katika kifaa chako na kuanza kuitumia. Utumiaji ni wa aina
yake kwani mwenye kifaa anaweza kuiwasha na pia kulinda uwashaji huo na nenosiri.
Yaani inamaanisha kama App hiyo ikiwashwa hakuna mtu anaeweza kuizima labda awe ni
Yule mwenye nenosiri.
0 comments:
Post a Comment