Tume inayohusika na kusimamia mifuko ya hisani imesema kuwa ni paund 14,115 sawa na shilingi za kitanzania milioni 43 ndizo zilizotumika kwenye mfuko huo nje ya paund milioni 1.7 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 5 za kitanzania zilizochangwa kwenye mfuko huo uitwao Didier Drogba Foundation ili kusaidia matatizo barani Afrika. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 38 ametishia kuchukua hatua kali za kisheria huku akilijia juu gazeti la Daily Mail ambalo limechapisha habari hiyo kwa kina.
Drogba ambaye kwa sasa anakipiga kunako ligi kuu ya nchini Canada kwenye klabu ya Montreal amesema kuwa kuutikisa mfuko huo ni kuhatarisha maisha ya watoto wengi barani Afrika ambao wanasaidiwa na mfuko huo.
Drogba ambaye amesema kuwa ametokea kwenye familia ya kimaskini, hawezi kuuhujumu mfuko huo ambapo ametaja mambo kadhaa mfuko iliyofanya ikiwemo kujenga hosptali, kusaidia yatima na kuinua sekta ya elimu.
0 comments:
Post a Comment